Lamentations 3:22-26


22 aKwa sababu ya upendo mkuu wa Bwana, hatuangamii,
kwa kuwa huruma zake hazikomi kamwe.

23 bNi mpya kila asubuhi,
uaminifu wako ni mkuu.

24 cNimeiambia nafsi yangu, “Bwana ni fungu langu,
kwa hiyo nitamngojea.”


25 d Bwana ni mwema kwa wale ambao tumaini lao ni kwake,
kwa yule ambaye humtafuta;

26 eni vyema kungojea kwa utulivu
kwa ajili ya wokovu wa Bwana.
Copyright information for SwhKC